Mtazamo Wangu....

Karibuni katika ukurasa huu mpya  wa Mtazamo Wangu ambao unajikita zaidi katika Majadiliano, Maoni, Ushauri pamoja na kuchambua Changamoto mbalimbali zinazo ikabili jamii yetu.
Kwa karibu zaidi ukurasa huu utaangalia yafuatayo; Jamii na Maendeleo, Uongozi na Viongozi  na Maendeleo na Vijana

Lengo kuu la ukurasa huu ni kuchangia katika kuboresha mjadala wa harakati za maendeleo yanayoleta mabadiliko kwa Jamii yetu.Hivyo basi karibuni wote mnaotembelea blog hii.  Pichani, vijana wakijishughulisha na biashara ndogondogo katika mji mdogo wa Chalinze mkoa wa Pwani wakiwadumia abiria waendao mikoani wakiwa ndani ya mabasi yapitayo mjini hapa.

Maswali ya msingi niliyo kumbana nayo katika safari yangu ya kelekea Tanga na kuiona hali hii juu ya vijana hawa ni kwamba, je jamii yetu inawaonaje vijana hawa hasa katika suala zima la maendeleo yao kiafya, kielimu kimaisha,

Je Mkukuta II  ni jibu la  hali  hii? Uongozi na viongozi wetu wanamikakati gani juu ya vijana hawa na jamii nzima? La mwisho kubwa ni nafasi ya vijana katika kuchangia mendeleo ya Taifa letu inapewa kipaumbele kwa kiasi gani?